GET /api/v0.1/hansard/entries/1502715/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502715,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502715/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ikitoka Upper House iende kwa National Assembly ambayo imekuwa na shida nyingi sana na magavana kwa sababu wanapata pesa nyingi kuliko zile zinazotengewa kaunti zetu . Constituency moja inapata Shilingi 150 milioni kwa MP mmoja. Isitoshe, wamejiongezea pesa za barabara. Wamejipitia Shilingi 60 milioni. Hao MPs wamejipatia Shilingi 30 milioni za kutengeneza stima.Kwa hivyo, shida ya hizi pesa za devolution si makosa ya President, ila ni makosa ya MP. Kwa hivo, ningependa kukosoa wanaopinga huu Mjadala. Tunafaa kukaa chini kwa sababu Bibilia inasema watu wawili hawawezi kutembea bila kuelewana. Tunafaa tuelewane na National Assembly ili tuweze k upatia watu wa mashinani fedha za kutosha juu ya economy ya counties. Mwisho, tumeona kuwa fedha hizi hazitoshi kwa sababu ya pending bills and pending wages zilizoachwa na wale magavana waliokuwako. Ningeomba countygovernors, fedha ambazo mnakusanya mashinani muongezee ili muweze kupata pesa zitakazosaidia kuongezea pesa hizi ambazo tumewapatia.Kwa mfano, nafurahia sana na Gavana wa County ya Embu. Embu County ilikuwa imepangiwa kukusanya Shilingi 900 milioni lakini yule gavana wa zamani alikuwa anakusanya Shilingi 350 milioni. Bw. Spika wa Muda, yule gavana yuko saa hii amefikisha Shilingi 750 milioni na ndio maana namuunga mkono. Hizo pesa ndizo magavana wanafuja. Gavana wa Kaunti ya Embu amefanya kazi nzuri lakini hajafikisha zile pesa zinafaa kutoka, angalau Shilingi bilioni moja ili kuongezea zile pesa zitatoka huku Seneti. Ninaomba ajifunze na zile kaunti zile zingine. Tumesikia kaunti nyingi zimetafuta njia za kukusanya ushuru kule mashinani. Ninashukuru pia Kaunti ya Embu na wale wafanyikazi wanaokusanya zile pesa na pia wafunge zile laini zilituharibia ndio tuone kama tutafika pahali panafaa. Bw. Spika wa Muda, kaunti zimekuwa na shida za hapa na pale kwanza upande wa hospitali. Ningeomba Serikali iweze kuangalia haya mambo. Kule Treasury pia kuna shida na ningeomba Waziri wa Fedha akubaliane na kaunti. Serikali ya Kenya Kwanza ilipoingia mamlakani, Rais wetu alisema kila mwezi mpaka kaunti zipate pesa na juzi tumesikia kwa miezi mitatu, kaunti hazijapata pesa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}