GET /api/v0.1/hansard/entries/1502742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502742,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502742/?format=api",
    "text_counter": 174,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, huu ni wakati wangu wa kwanza kutoa maoni yangu kuhusu sheria hii ambayo tumetunga juzi kuhusu makadirio ya fedha kwenye Serikali Kuu na zile za kaunti. Nilipokuwa nikichangia kwenye Kamati ya Usuluhishi, nilikuwa mmoja wa wale wabunge wa Seneti ambao walikataa. Maoni yangu ni kuwa zile pesa ambazo kaunti zilikuwa zimepewa, zilikuwa zimetosha na hakukuwa na haja ya kuziondoa kwa sababu zile pesa ambazo Serikali Kuu inazitumia kiasi chake ni kikubwa kwani ni asilimia 85. Tafadhali hakikisha ugatue yale majukumu ambayo gatuzi zote zinapaswa kufanya na hela zao mwaka ujao. Sasa tumefanya uangalizi wetu. Tumekagua vitabu vyote vya kaunti zote 47. Sasa tumefika mwaka wa 2023/2024. Kwa Kimombo tunasema tuko"
}