GET /api/v0.1/hansard/entries/1502744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502744/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Tunafanya hivi kwa sababu katika gatuzi zetu ndiko umaskini mwingi uko. Watu wengi wanaishi kwa kaunti zetu. Hivyo basi, huko mashinani ndiko tunahitaji barabara nyingi, maji, ukulima na madaktari. Jambo la kwanza ambalo sisi kama Seneti tunapaswa kufanya ni kuhakikisha tumemuuliza Rais kwa heshima ahakikishe kuwa amegatua fedha na yale majukumu ambayo yamegawiwa kaunti. Pili, magavana wamekuwa wakisema kila wakati kuwa hawajapata pesa kutoka kwa Serikali na pia mishahara haijawafikia. Lakini, tungependa kuwaambia ndugu zetu magavana kuwa Wakenya sio wajinga sasa. Wakenya wanajua ni wakati gani Serikali inatoa pesa na wakati ambao fedha hizi hufika kwa gatuzi zetu mashinani. Magavana wanapopata hizi pesa wanatakiwa kuzitumia vizuri ili zifanye kazi. Ninapozungumza sasa hivi, kwa Hazina ya Fedha ya Kaunti County Revenue"
}