GET /api/v0.1/hansard/entries/1502746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502746,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502746/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "katika Kaunti yangu ya Kisii, kuna shillingi bilioni tisa na laki tatu. Lakini, Gavana wangu amekuwa akiambia watu hakuna pesa. Waliokuwa wakandarasi hawajalipwa, wafanyikazi wa kaunti wanafutwa kazi na wengine kuajiriwa. Hakuna mambo yanaendelea. Hakuna barabara na mvua kwa sasa imenyesha. Ukiangalia zile shida ziko kwa kaunti zote kama vile Sen. Cherarkey alikuwa anasema, kwa heshima utamwambia Gavana wako ya kwamba pesa mimi ndimi nimeuliza, nikazichunga, zikaja na sasa ziko kwa account . Tafadhali, tumia hizi pesa usaidie watu wetu. Ukifanya hivyo, anakutafutia goons . Wanakuja na panga na wengine na bunduki. Ooh, huyo Seneta anataka kutunyang’anya ugavana wetu, ooh, huyo Seneta ndiye mwizi. Ningependa kuambia magavana wetu hatuna vita na wao. Wengine wetu hata hatutaki kuwa magavana. Kaunti yangu ya Kisii napata kila mwaka shilingi bilioni kumi na tano. Kwa miaka miwili Kisii imepata bilioni thelathini. Ukitoa pesa za mishahara shilingi bilioni sita na nusu, bilioni kumi na tatu ndizo zimeenda kwa mishahara. Shilingi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}