GET /api/v0.1/hansard/entries/1502747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502747,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502747/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "zingine bilioni kumi na sita ama kumi na mbili ndizo hubaki za kuwafanyia wananchi kazi. Hamna madawa hospitalini, miradi iliyokuwa inaendelea ya maji haifanyiki, pesa zote zinazotoka kwa donors zimesimamishwa katika Kaunti ya Kisii, kwa sababu vigezo vyote ambavyo vimekwa na wafadhili vimekiukwa. Gavana alipoingia huko alitoa wale waliokuwa wakitia signature na kuweka watu wake. Hakujua sheria inasema hawezi kufanya hivyo. Ukiuliza walimu wa shule za chekechea, hawajalipwa mishahara. Wengine mishahara yao ni minimum wage . Utamuajiri aje mtu afunze mtoto wako kutoka darasa la kwanza hadi la tatu au la nne, ilhali unamlipa shilingi elfu saba? Huyu ni mtu amesoma na hata wengine hadi chuo kikuu. Wale Community Health Promoters (CHPs) wa vijijini Serikali iliahidi kutenga pesa watakazokuwa wanapata. Je, nini kimefanyika? Katika Kaunti ya Kisii, CPHs hawajalipwa ilhali kwa county revenue fund ya Kisii, kuna shilingi bilioni sita. Sasa hizi ndizo shida zetu hapa Kenya. Kuna ufisadi, wizi na lack of management . Bw. Spika wa Muda, tunapaswa kujiuliza kama Wakenya swali hili. Iwapo mtu anataka kuwa gavana, anafaa kwenda shule gani kwa sababu kazi imeshinda wengi wao? Mtu akichaguliwa kuwa gavana, kazi ya kwanza ni kuwafuta kazi watu walioajiriwa na gavana aliyemtangulia kwa sababu si wa ukoo wake. Anavunja sheria kwa kuajiri watu wa ukoo wake kwa sababu walimpigia kura. Hiyo ni njia ya kuwaambia kuwa yeye ni mzuri lakini gavana aliyemtangulia alikuwa mbaya. Watu hao wote ni Wakisii. Wote ni Wakenya na wanalipa ushuru. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatukera. Tumefika mahali ambapo lazima tujiulize kama Wakenya. Je, tutalinda vipi pesa ambazo wananchi wa Kenya wanatoa kupitia kwa ushuru? Namheshimu sana Gavana wa Kakamega. Nilikuwa katika mkutano huo na sikutaka kujibu. Alisema kuwa the Controller of Budget (CoB) ndiye anamnyima pesa. Ni kweli kuwa baadhi ya magavana wamekatazwa kutoa pesa na Msimamizi wa Bajeti. Vile Sen. Cherarkey alivyosema, wakiwa na CIDPs, wanaweza kutumia"
}