GET /api/v0.1/hansard/entries/1502754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502754,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502754/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "wanayomiliki, lakini hatuwezi kuwa na huruma kwa watu wetu? Ni zaidi ya miaka 60 tangu tupate Uhuru, lakini watu wengine hawana maji ya kunywa. Tulikwenda kule Turkana ambako anatoka Sen. Lomenen. Kufikia sasa, Turkana imepata shilingi bilioni 110, ilhali watu hawana maji ya kunywa mijini baada ya miaka kumi tangu kuwa na ugatuzi. Ni kinaya kuwa hali ni hiyo ilhali kuna maji mengi kutoka Mto Turkwel. Kinachotakikana ni maji kusambazwa kwa wananchi. Wamepata shilingi bilioni 110, ilhali watu hawana maji! Kwa miaka miwili sasa, Kaunti yangu ya Kisii imepata shilingi bilioni 32. Hata hivyo, ukienda kule hamna chochote. Uwanja wa Michezo wa Kisii haujatengenezwa na hakuna dawa katika hosipitali za Kisii na maji. Gavana anasema kuwa own sourcerevenue imeongezeka hadi asilimia 75 na sasa wanatarajia shilingi milioni 800. Wanafuja"
}