GET /api/v0.1/hansard/entries/1503599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1503599,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1503599/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Naibu Spika, Naunga mkono uteuzi wa maafisa wa IPOA, ijapokuwa bado nina shauku katika utekelezaji wa Katiba ambayo inatambua maeneo yaliyo Kenya. Wakati Mhe. Osoro alikuwa anachangia, alitaja maeneo ya Bonde la Ufa na Mlima Kenya lakini, kwa ufasaha wake, hakuzungumzia eneo la Pwani kwa sababu anajua kwamba ni eneo moja ambalo uteuzi kama huu unapotokea, kawaida huwa halitajwi na kutambulika. Kwa hivyo, nikiunga mkono, nataka tuzingatie Katiba inavyotaka, kwamba maeneo ni nane. Iwapo nafasi ni nane, tuwe na uteuzi kutoka kila eneo."
}