GET /api/v0.1/hansard/entries/1503784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1503784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1503784/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Ni vizuri wenzangu wasome Kanuni za Kudumu za Bunge ili wajue ni wakati upi mtu anaweza kupatiwa nafasi ya kuzungumza, na ni wakati upi asipatiwe. Sijazungumza katika Hoja hii na, kwa hivyo, nina haki yangu ya kutoa maoni. Nakubaliana na Ripoti ambayo imeletwa ya uteuzi wa Mwenyekiti, Mhe. Rehema Dida Jaldesa, na mwanachama, Michael Nzomo Mbithuka. Naunga mkono Hoja hii ili waweze kuteuliwa kama inavyostahili. Ningetaka kutilia mkazo utendaji kazi wa hizo tume ambazo zimeteuliwa, haswa tukiangalia tume mbili mtawalia na Wizara inayohusika ya jinsia: Tume ya Jinsia na Usawa na Tume ya Uwiano. Kama Kiongozi wa Wengi Bungeni alivyotanguliza, kuna tatizo kwa sababu majukumu ya Tume hizo mbili yanatatizana. Katika Ripoti iliyotangulia hapo mwanzo ya National Dialogue Committee (NADCO), wananchi walitoa mapendekezo kwamba Tume hizo zivunjiliwe mbali. Taratibu za kufanya hivyo ni ndefu. Katika hili Bunge, tukae na tuwapatie majukumu. Kila Tume iwe na majukumu maalum ambayo hayaingiliani na zile tume zingine. Hilo litaweza kutatua kwa upande mmoja tatizo ambalo limezungumziwa kwa kirefu kwamba Tume hizo hazipatiwi fedha za kutosha. Fedha hazitoshi kwa sababu wamepewa majukumu ambayo kila mtu anasema ni yake, na yakienda vibaya, mwingine anasema siyo yake. Inatakikana Bunge hili, kwa haraka,"
}