GET /api/v0.1/hansard/entries/1504308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1504308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1504308/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Asante sana kwa kunipatia nafasi na mimi pia niweze kuunga mkono uteuzi wa Seneta Wamatangi. Majina ya Seneta nayo… Nampongeza Senator Wamatinga kwa kuteuliwa. Ningependa kumuelezea kuwa akishateuliwa, awashikilie Wabunge. Maswala yetu kama Wabunge yanaangaliwa na Makamishna wa Parliamentary Service . Tunawasihi wafanye usawa kwa kila jambo. Kuna Wabunge wanaolia na kutatizika juu ya maswala yanayowahusu. Tunawasihi tu, mkiteuliwa, na nyinyi mkumbuke wenzenu. Mara kwa mara, sisi huwapigia kura ili mpate nafasi ya kuhudumu katika hili Bunge na kuangalia maswala ya Wabunge bila upendeleo. Ninamuombea Mungu ili apate mafanikio kwa uteule wake. Ninamshukuru sana Mhe. Rais, Daktari William Samoei Ruto kwa yale aliyotueleza jinsi anavyoendeleza uchumi. Kwa hivyo na wao, wasimkatishe tamaa; inafaa washike kasi na waangalie Wabunge na maswala yao maana kuna malalamishi mengi yanayotoka kwa Wabunge. Ninavyoongea, niko kama sauti ya Wabunge kwa ujumla. Makamishna wasiangazie mambo yao ya kibinafsi. Kuna wale wanaofanya kazi nzuri, na tunawapongeza lakini wengine, wanajiangalia kibinafsi. Tunawasihi waangalie nafasi ya Wabunge pia. Vile tumechaguliwa, nasi tuko na mambo mengi ambayo tungependa yaangaliliwe."
}