GET /api/v0.1/hansard/entries/1505499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1505499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505499/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kwa mfano, Nairobi City County, yatarajiwa kukusanya zaidi ya Shilingi 60 bilioni, lakini mpaka sasa wako katika Shilingi 12 bilioni au 13 bilioni. Mombasa County wana uwezo wa kukusanya Shilingi 10 bilioni, lakini sasa tuko kwa bilioni tano, nusu ya uwezo wake. Kwa hivyo, ipo haja ya kaunti zetu, si kila mwaka wapige kelele kuwa pesa zinazokuja kutoka Serikali Kuu ni kidogo. Wanafanya nini kukusanya hizi fedha? Hizi fedha zikifika kwao zinaleta maendeleo? Hospitali hazina madaktari wa kutosha na vile vile wafanyakazi katika masoko hawako. Kwa hivo, ni lazima county zetu pia zijitahidi. Isiwe kwamba lawama inaenda kwa Serikali Kuu kila siku. Ndio, lazima tulaumu Serikali Kuu kwa sababu wao ndio wenye mfuko mkubwa lakini kaunti zetu lazima zijitahidi. Kwa hayo mengi, Bw. Naibu Spika, naunga mkono Ripoti hii."
}