GET /api/v0.1/hansard/entries/1505531/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1505531,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505531/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii kuchangia kuhusu makubaliano kati ya Seneti na Bunge la Taifa kuhusu mgao wa fedha utakaoafiki maendeleo katika nchi ya Kenya. Siku zilizopita, Maseneta wamekuwa wakijihusisha na mchakato wa kutia kwenye mizani utekelezaji wa kazi au maendeleo katika kaunti mbalimbali katika kamati mbalimbali. Baadhi ya magavana waliokuja, baadhi yao walikuwa wangwana na kukubali makosa lakini wengine walikana makosa ila sisi tuliwakosoa. Fauka ya hayo, kuna wale ambao walikuwa na kiburi na vichwa butu. Walikuwa wanadhani na kusema ya kwamba hakuna chochote Seneti inawasaidia. Nashukuru Maseneta waliosimama kidete na kusema ya kwamba fedha zinazoenda katika kaunti zetu zisipungue chini ya shilling billion mia nne. Shinikizo ama ukosefu wa pesa katika kaunti uliwalazimu magavana kukubali ya kwamba Seneti ipo na itaendelea kuwepo kutetea pesa zinazoenda katika kaunti na vilevile kuchunga maslahi ya kaunti zetu. Linalosababisha ninyanyuke na kutoa Hoja zangu ni kwamba Kaunti ya Bungoma ni mojawapo ya kaunti ambazo zimekuwa na fedha chache. Gavana amekuwa akisema hana pesa za kutekeleza miradi ya maendeleo. Ni sawa, lakini sasa tumemaliza shida iliyokuwepo ya kukubaliana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}