GET /api/v0.1/hansard/entries/1505532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1505532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505532/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Natarajia kule mashinani Bungoma, maeneo ya mazoezi ya wanariadha kule Mlima Elgon yatakamilika. Imechukua zaidi ya miaka 10 eneo hilo kujengwa na fedha ambazo Bungoma imepata kufikia sasa ambazo ni zaidi ya bilioni thelathini na sita. Seneti inapaswa kujiuliza iwapo miradi ambayo magavana wanajishughulisha nayo itakamilishwa katika awamu yao ya uongozi ama watapata kiinua mgongo na kuwaachia magavana watakaokuja shida na madeni jinsi tunavyoona. Bw. Naibu Spika, ukiangalia sekta ya afya, kule Bungoma, hakuna dawa kwenye hospitali. Vile vile, kuna mijengo na miundombinu ambayo haijakamilika. Nyingi ya mijengo hiyo ilianzishwa na magavana waliokuweko. Kile tunadai ni kuona magavana wakikamilisha miradi ya maendeleo ambayo ipo. Hatutaki kuona magofu ya miradi katika kaunti zetu. Vile vile, sekta ya ukulima imeathirika pakubwa na utepetevu wa baadhi ya mawaziri na magavana katika Kenya hii. Tumekubali kuwapa pesa lakini ni lazima uwajibikaji udhihirike na uonekane kadamnasi ya umma. Nakubaliana na ripoti ya Kamati ya Uwiano ambayo ilihusisha Seneti pamoja na Bunge la Taifa. Nilileta Taarifa iliyoelekezwa kwenye Kamati ya Barabara, Uchukuzi na Makazi na sasa karibu miezi saba imepita. Juzi kule Bungoma, kuna watu waliodai kuwa--- Kuna barabara ya foleni mbili au tatu ambayo ilijengwa na baadhi ya Maseneta wanajua. Fedha zilitoka katika awamu iliyopita. Badala ya kukamilisha barabara hiyo, walianza kuipaka rangi. Naomba kamati ambazo ziko hapa zisiwe za kuimbia magavana nyimbo kama watoto wa chekechea. Lazima magavana wawajibike, kazi iliyotendeka ionekane na malipo yanayotolewa yaonekane kuwa yametolewa kwa haki. Ninatarajia kwamba tunaposonga mbele, tutaweza kupewa nguvu na uwezo unaostahili kwa sababu hata sisi Maseneta tumekuwa kama makachero katika Benki Kuu ya Kenya ambapo kile tunacho ni Bibilia na rosari. Tuonapo wezi, tunasema kwamba iwe jinsi Mungu alivyopanga. Hafla ama maombi kama hayo hayapaswi kuwa tu ya Maseneta. Inatakikana tukiona nia ya mwizi tunapambana nayo mapema. Naomba kwamba tunapomaliza mchakato huu, fedha ziende katika kaunti zetu nasi tuziandame ili kuhakikisha kuwa magavana wanafanya kazi, wanakandarasi kule mashinani wanapewa nafasi na watoto wetu wanapewa kazi pasipo kubaguliwa jinsi ilivyo. Tunapoingia kwenye msimu wa Krismasi, ningependa tuone mabadiliko. Hatufai kuwa na mtamauko bali maono mazuri ambayo yatatusukuma kwa mwaka unaokuja ili mwaka huo tuwe na mapenzi na umoja katika mustakabali wa nchi ya Kenya. Bw. Naibu Spika, naunga mkono makubaliano ya Kamati ya Uwiano. Asante sana. "
}