GET /api/v0.1/hansard/entries/1505645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1505645,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505645/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, Mswada wa pamba ambao uko mbele yetu ulimaliziwa katika Bunge la Seneti na ukaenda Bunge la Taifa ili uweze kuzingatiwa baada ya kufanya misururu ya mikutano na uhamasishaji wa umma katika sehemu tofauti na Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ya Seneti kuleta ripoti katika Seneti. Ilipoenda kule, kuna marekebisho ambayo Bunge laTaifa limeomba yafanywe na ukarudishwa tena kwa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati. Tulikaa chini na tukavalia njuga swala hilo na tukaangalia mambo yote ambayo yanafaa kuangaliwa, na tukakubaliana kwamba, marekebisho yote yaliyotoka Bunge la Taifa yanafaa kuzingatiwa. Kwa hivyo, hakuna Seneta aliyekuja kupinga marekebisho yaliyotoka Bunge la Taifa. Hivyo ni kusema kwamba, ripoti ambayo tuliandika na kuileta hapa Bunge la Seneti, ipo na hivyo nimesema, ndivyo inasema kwa kwamba, tunakubaliana na marekebisho yaliyo kwenye ratiba ya Seneti. Bw. Spika wa Muda, huu Mswada ni muhimu sana kwa sababu ukizingatia maeneo ya kiuchumi yanayoitwa Export Processing Zones (EPZ) ambapo viwanda vingi vinavyotengeneza nguo ambazo zinazotokana na pamba. Leo hii ni kusema, viwanda vile wananunua vitambara kutoka nchi za nje, sana sana, nchi ya Bangladesh. Tulienda gatuzi la Busia na tukawa na mkutano. Ninachukua nafasi kushukuru Seneta wa Busia, Mhe. Okiya Omtatah, kwa sababu alitupea nafasi nzuri na kukaa na kuongea na wana-Busia. Serikali imejenga kiwanda kipya cha kushugulikia pamba na kutoa nguo. Shida iliyokuweko ni kwamba, hakujakuwa na sheria muhimu ambayo inaratibu biashara ya ukuzaji wa pamba na uuzaji wa pamba inafaa kufanywa. Tulifikikiria ni vizuri Mswada ulioletwa mbele yetu na Seneta Beth Syengo tuuzingatie tuifanye msingi katika ile biashara ya kilimo ili iwe ni kilimo biashara na sio bora kilimo. Maeneo yote nchini ukizunguka, kuanzia Nyanza, kwenda Magharibi mwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}