GET /api/v0.1/hansard/entries/1505646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1505646,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505646/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "nchi, Bonda la Ufa, maeneo ya Kati, Ukambani na uende mpaka Lamu katika eneo la Pwani, pamba kwa sababu inastahimili ukame, inaweza kukuzwa katika sehemu nyingi. Ni kitega uchumi kizuri na kama tutawekesha na kuhakikisha kwamba kuna mtaji wa kukuza pamba, pembejeo zinapatikana na mbegu zinaitwa za BT, ambazo kilo moja ni zaidi ya Shilingi 7,000 lakini ni pamba nzuri sana ikipewa wakulima. Tulionelea ikiwa wakulima watapewa nafasi na pembejeo, watanufaika pakubwa na pamba. Bw. Spika wa Muda, pamba ni mmea ambao una maana sana kwa sababu, ukitoa ile pembe kwa kimombo inaitwa lint, itatengeneza nguo. Ukitoa mbegu ya ndani na kuifinya, itatoka mafuta. Hayo mafuta kwa kimombo yanaitwa biodiesel na hata kuna mafuta ya kupikia. Ile inabaki, cotton seed cake inakuwa ni kiungo muhimu katika kutengeneza vyakula ambavyo vinalisha wanyama, kwa wengi ambao ni wakulima wa ng’ombe na mbuzi wa mazima, nguruwe na hata kuku. Hivyo ni kusema kwamba, pamba ni mmea ambao kila kitu kinachotolewa kwa pamba kinatumika vilivyo na inaweza kuwa kitegauchumi kikubwa kama tunaweza kushughulikia pamba na kuhakikisha viwanda vinatosha. Jambo lilikuwa kubwa tulipokuwa tukizunguka ni kwamba, viwanda vingi vya pamba au ginneries vimevunjika na vingine viliuzwa. Vingine pia, wakiritimba walikuja wakavamia mashamba na wakayachukua kwa njia ya ulaghai. Mfano mzuri ni kiwanda cha pamba kilichokuwa mahali kunaitwa Ngurubani katika gatuzi la Kirinyaga. Utapata mashine hazipo, ziliibiwa na kiwanja hakiko, kilienda. Lakini, kama Kamati, tuna mpango kwamba, Mswada huu utakapopita kwa sababu hii ndio safari ya mwisho ili uweze kupita, tutazunguka tukiangalia hivi viwanda. Pia, tutahusisha Wizara ya Ardhi kuhakikisha kwamba, yale mashamba yalikuwa ya serikali ambapo, pamba ilikuwa inaenda pale kushugulikiwa na kusaidia mkulima, yamerudishwa ili tuhakikishe kwamba, mashine zimerudishwa na wakulima Kenya nzima wafaidike. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia maongezi au, unapotoka hapa na uende sehemu kame kama Kitui, Makueni, Busia au Homa Bay, mahali Seneta Kajwang’ ametoka, swali unaloulizwa na wale wananchi ni kwamba, tunasikia watu wakitaja majani chai, kahawa na miwa, lakini, chetu ni kipi katika hizi gatuzi kwa sababu, sisi ni walipa kodi ambao tunafaa kushikiliwa na kupewa mitaji na kusamehewa mikopo ili sisi pia tusikie ni kama Wakenya? Kwa hivyo, pamba tunayoongelea siku ya leo ni mojawapo ya mmea ambao unaweza kustawisha na kusawazisha Wakenya wengi katika Kenya hii ili kila Mkenya asikie ni Mkenya na hajatengwa. Lamu inakuza pamba. Ukienda Kilifi utapata wanakuza pamba. Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati hii. Kwa kudura zake Mwenyezi Mungu, tutahakikisha kwamba Mswada unaowasilishwa kila sehemu nchini, kutakuwa na kitegauchumi."
}