GET /api/v0.1/hansard/entries/1505649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1505649,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505649/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Samahani, Bw. Spika wa Muda. Nitahakikisha nitafuatilia maagizo hayo. Nilikuwa namalizia kwa kusema ya kwamba, mmea wa pamba ni mojawapo ya mimea ambayo inasawasisha jamiii nyingi nchini. Wakati kuna watu ambao wanasamehewa mikopo, kuna watu wanaopewa mitaji, iwe kwamba kila Mkenya ana mmea unaompatia pesa za kujikimu. Ukiangalia takwimu ya mahali ambapo pamba inapandwa, pamba ni mmea unaoweza kustahimili ukame. Sehemu nyingi nchini zinaweza kukuzwa pamba. Pia, katika Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuna miswada ambayo tutawasilisha kuhusu jamii za wafugaji ili kuhakikisha kwamba wananufaika na kilimo biashara. Mswada huu utakapotiwa sahihi na Rais wa Jamuhuri ya Kenya utakuwa ni Mswada wa tatu ambao umepitia katika Kamati ya Kilimo Mifugo na Uvuvi katika Bunge la Seneti. Tumehusika vilivyo kuhakikisha imepita. Mswada wa miwa umepita. Aliyekuwa mdhamini mwenza katika Mswada huu ni Sen. Wafula ambaye ni wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kuna Mswada wa kahawa ambao utasomwa kwa mara ya tatu katika Bunge hii. Pia kuna Mswada ambao umeletwa na Sen. Beth Syengo ambaye ni wa Kamati ya ukulima Mifugo na Uvuvi ambao tunamalizia. Kwa jumla, tuko na Miswada 15 ambayo imewasilishwa na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Nitakuwa kalili wa akili kama sitasema kuwa kuna Mswada mmoja ambao ulituuma sana kama Kamati. Huu ni Mswada ambao ulikuwa unahusu ndengu ambao ulikuwa umeletwa na Sen. Wambua. Ndengu ni kama pamba inakuzwa kila mahali. Alipochukua nafasi kuongea na Wabunge wa Bunge la Kitaifa kujua kwa nini Mswada ulififia na ukafa kwa njia ambayo haikueleweka, wengi waliokuwa wanaongea, walikuwa wanaongea kwa hali ya kutojua. Ungemsikia Mbunge akisema kuwa kuna Mswada wa ndengu ambapo mtu atalipishwa shilingi1 millioni. Athari ya kufanya siasa na Miswada ambayo inapita katika Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ni moja. Tulipokaa kwa sababu ya Mswada wa miwa hakukuwa na siasa duni. Mswada huu Rais alipiga sahihi. Mswada wa kahawa haujakuwa na siasa. Hivi karibuni utatiwa kidole kwa sababu unasomwa kwa mara ya tatu. Mswada wa pamba haujatiwa siasa. Wale wakulima wa ndengu wamepoteza nafasi muhimu sana. Hivi sasa, Serikali inapambana kuhakikisha kwamba kuna lishe bora na usalama wa chakula nchini. Tuna changamoto kama Seneti kwani lazima tuhakikishe kwamba wananchi wanafahamu kazi yetu kwa kuieleza waziwazi. Kuna watu wanatumia Miswada inayokuja kwenye Bunge la Kitaifa kupigana kisiasa. Wanafikiria kuwa Mbunge akipitisha Mswada atapata umaarufu. Wanasahau ya kwamba wanaopitisha Miswada ni Wakenya. Kwa mfano, nimetoka eneo la Kirinyaga. Sisi hatukuzi miwa. Mswada huu ulipokuja kwenye Kamati, nilikumbuka kuwa wakulima wa miwa wamekuwa katika lindi la umaskini kwa miaka ambayo hatuwezi kuhesabu. Tulipoona nyuso za wazee huko Chemilil ambao wamelima miwa na bado ni maskini, na kusikia kilio cha wakulima wa miwa ambao watoto wao hawasomi, wale afya zao zimedhoofika na bado ni wakulima na wameendelea kulima. Ukiwa na utu na ukiwa kiongozi lazima ulivalie njuga jambo lile kuhakikisha kwamba watu wale wamepata haki yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}