GET /api/v0.1/hansard/entries/1505650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1505650,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1505650/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Wakati Rais alisema kuwa Mswada wa Sukari uko hapa uzingatiwe, tulichoma mafuta usiku kucha na mchana kutwa. Mimi kama Mwenyekiti mwenza Mheshimiwa Emanuel Wangwe tukakaa chini na kuhakikisha kuwa tumemaliza kushughulikia Mswada huo. Tunapoongea, kuna matumaini katika wakulima wa miwa, kahawa na majani chai. Kwani kama Seneta wa Bomet umeleta Mswada kujaribu kulainisha mambo ya kilimo cha chai. Matumaini ya wakulima wa ndengu yako wapi? Matumaini ya wakulima wa pamba yako wapi? Kutakuwa na matumaini kama tutakuja na kuhakikisha kwamba Miswada kama hii inapita bila siasa ambazo hazina maana. Nikimalizia, Waswahili husema wavuvi wa pweza hukutana mwambani. Sisi kama Maseneta tukutane hapa ili mwamba wetu, tuunge mkono Mswada huu na marekembisho yote ili wakulima wa pamba wapate nafasi ya kuendelea na wakulima wao na waweze kufaidika. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}