GET /api/v0.1/hansard/entries/1506412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506412,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506412/?format=api",
"text_counter": 183,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": "(Matuga, ANC) : Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa. Langu kwanza ni kumpongeza Mhe. Mwadime, aliyekuwa Mbunge wa Mwatate, kwa kuanzisha Mswada huu. Wajua sasa hivi anaitwa His Excellency Governor wa Taita Taveta. Kwa hivyo, nampatia pongezi. Pili, nampongeza Mhe. Daktari Makali Mulu kwa kuuregesha Mswada huu muhimu. Nahuzunika na wale ambao walitoa nguvu na maarifa yao, na uaminifu wao kwa hii Serikali bila kuiba. Mswada huu siuangalii tu kama utakaoboresha maisha, bali pia kama utakaosaidia kupunguza jinamizi la wizi katika Serikali. Wafanyikazi wengi si Wabunge tu bali hata wale walio kule nje, wakati wajuapo kuwa wanaenda kustaafu, huwa na wasiwasi wataishi vipi. Si ajabu kuwa baadhi ya Wabunge huwa na hilo shaka kwamba, wasiporudi na wana mishahara na bima ya kulazwa hospitalini, kutibiwa macho na meno itakuwaje. Kwa hivyo, huu Mswada ninauangalia kwa kipimo cha kuweza kupunguza wizi na matumizi mabaya ya pesa za umma. Endapo Mbunge atajua kuwa hata akistaafu na hatakuwa Bungeni ataishi maisha ya heshima na pesa atakayopata itamwezesha kukimu maisha yake, hatakuwa na haja ya kuanza kufikiria ni vipi atachukua mali ya umma aiweke kando kwa minajili ya wakati atakapostaafu au hatakuwa Bungeni."
}