GET /api/v0.1/hansard/entries/1506414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506414,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506414/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": "Jambo ambalo pia ni muhimu katika huu Mswada ni suala la kuwa kwa mara ya kwanza, itatambulika kwamba kuna uwezekano wa mwanamke kuwa Mbunge. Akiwa hai, ni wazi kuwa mama huyo ataishi raha mustarehe na anajua anavyofanya. Endapo mama huyo atatuacha – na hilo ni jambo la kawaida kwa sababu kama kuna uhakika wowote maishani ni kuuacha ulimwengu huu – basi yule bwana aliyekuwa anaishi naye pia anufaike na yale marupurupu ambayo kama ingekuwa ni mume ameaga dunia na kumuacha mkewe, angeweza kunufaika nayo. Kwa hivyo, Mswada huu ni muhimu na ninauunga mkono kwa dhati. Ahsante, Mheshimiwa Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii."
}