GET /api/v0.1/hansard/entries/1506440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506440,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506440/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi pia nichangie Mswada ulioletwa Bunge la Taifa na Mhe. Makali Mulu. Nampongeza. Mswada huu unaongea kuhusu masuala ya Wabunge. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unashughulikia masuala ya Wabunge. Tunaelewa tunapochaguliwa kufika hapa Bunge, tunatekeleza kazi ya wananchi. Tunatunga sheria kwa niaba ya wananchi wa Kenya. Kwa hivyo, mara nyingi, hatuna nafasi kubwa sana ya kujijenga kiuchumi ama kufanya Biashara. Tulifika Bunge hili baada ya uchaguzi na wito wa Mungu kuongoza watu. Kwa hivyo, tusipoongea mambo ambayo yanatuhusu kama waheshimiwa, ikifika wakati hatutarudi katika Bunge hili ama tumestaafu, ni vizuri sana tuangalie maslahi yetu tukiwa nyumbani. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unaongea kuhusu bima ya matibabu. Hakuna kitu kibaya kama kuchaguliwa, na unaingia katika kiwango kingine cha maisha. Baadaye ukienda nyumbani, unakosa kulipa bili za hospitali. Kwa hivyo, Mswada huu unagusa kitu cha maana katika maisha ya Wabunge na wale watafaidika."
}