GET /api/v0.1/hansard/entries/1506441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506441,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506441/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": "Kitu cha pili ambacho kimefanya niunge mkono Mswada huu ni kwamba pesa ambazo zitakuwa zikikatwa zitatoka kwa mishahara yetu, na zitaenda kwa Parliamentary Service Commission. Tume ya Bunge itaiwa na kuiangalia, ama waipeleke direct kwa NationalTreasury . Ninasema hivi kwa sababu mara nyingi watu ambao wanaulizia pension yao wanakua na shida sana. Kupata hiyo pension inachukua muda, na ni kwa sababu hatujui ni utaratibu gani Wizara ya National Treasury and Economic Planning inatumia, ili wanachelewesha pesa ama wanaiweka sana hiyo pesa ambayo wananchi wa Kenya wanataka kujisaidia nayo. Kwa hivyo, pension ya Wajumbe ikiwekwa, iwekwe chini ya Tume ya Bunge kwa sababu utaratibu wao utakuwa rahisi sana."
}