GET /api/v0.1/hansard/entries/1506478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1506478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506478/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Tandaza amesema vizuri sana kuwa mti huo unaweza kutumika katika upande wa vipodozi, kutengeneza nyuzi zinazotumika kusuka, na katika mambo ya utamaduni. Mhe. Tandaza amefanya jambo la maana sana kuileta Hoja hii. Ameeleza kuwa kuna kiwanda cha kibinafsi kinachounda vitu kutokana na mti huo. Serikali inapaswa iingilie kati kuona ni jinsi gani ambayo kiwanda hicho kinaweza kufanywa large scale ili wananchi wanaounda vitu kutokana na mti huo wainuke. Mheshimiwa wa Matuga amezungumzia hayo kwa sababu tumewaona viongozi wenzetu kutoka kule Meru na sehemu nyingine wakijaribu ku- schedule miti iliyo katika sehemu zao ili watu wao wafaidike. Sisi pia tunaunga mkono mambo hayo, kwa sababu tunataka biashara ya mrangi ikolee vizuri. Sikupata nafasi ya kuchangia Mswada tuliozungumzia kuhusu pensheni ya Wabunge waliostaafu, lakini wengine wanaweza kuingia katika biashara hiyo ya mrangi, na ndio maana tunaunga mkono mambo hayo. Wanaweza kujisaidia katika maisha yao na ya watoto wao. Biashara ndiyo kitu peke yake kinachoweza kuwalinda Wabunge waliostaafu. Ni muhimu watu waweze kujikimu wenyewe kibiashara. Mswada uliopita ulizungumzia jinsi Mbunge anapokuwa Bungeni anathaminika, lakini akiacha kuwa Mbunge, tunamwona hapa mlangoni akizunguka katika njia za kutamausha. Wengine wanastaafu na wako na watoto wakorofi wanaowafanya wafe mapema kwa kuwasumbua, kwa sababu hawana kitu na hawawezi kuwasaidia."
}