GET /api/v0.1/hansard/entries/1506479/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1506479,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506479/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, hivi karibuni, wewe na watu wengine wengi mtakuwa kule Mombasa kwa Michezo ya Bunge ya Afrika Mashariki . Wengi wa kutoka huku bara wakija kule Mombasa, huuliza biryani iko wapi. Rangi ya biryani inatokana na mti huu wa mrangi. Usiwe na shida sana, Mhe. Spika wa Muda. Tutawakaribisha watu wote watakaokuja Mombasa. Watakula biryani ya mbuzi au ya ng’ombe iliyochanganywa na mti huo wa Bixa au mrangi, na vile vile biryani ya jodari. Mkija, tutawaonyesha utaalamu wetu wa kuutumia mti wa mrangi. Mti huo usitumike tu kupika biryani za mitaani, lakini utumike kwa export ama kutumwa nje ili biashara ipanuke. Tuko na Port . Kina mama, vijana na wazee wetu wajiunge pamoja katika vikundi, na Serikali iwapatie pesa ili wafanye biashara kama wafanyibiashara wengine. Mwishowe, itabidi nizungumze kwa njia ambayo italeta utata kidogo. Katika kila sehemu au region, watu wananufaika kwa miti inayotokamana na sehemu zao, kwa mfano, mti wa kahawa. Serikali inafanya juhudi kuangalia vile itawasimamia watu"
}