GET /api/v0.1/hansard/entries/1506481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1506481,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506481/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "hao ili waweze kuendelea. Katika sehemu zingine, watu wanaendelea kunufaika na parachichi pia. Serikali ya Kauti ya Narok inanufaika kutokana na mbuga za wanyama zilizoko Maasai Mara na sehemu zingine. Mti wetu sisi watu wa Kilindini ni Bandari, lakini haijatunufaisha inavyohitajika. Tunahitaji Serikali iingilie kati ili nasi tupate manufaa kutokana na Bandari yetu kama natural resource au mti unaomea kwa nguvu za Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye ameleta na kutupatia maji. Vilevile, tunataka mti huu wa mrangi utuinue kama vile watu wa majani chai, kahawa na parachichi wanavyoinuliwa na miti yao, ili tuone makundi ya watu wa Pwani wakijikusanya pamoja kusafirisha mti wa mrangi kwa kupitia vyombo, ili nao pia wawe matajiri. Tunataka watu wawe matajiri, ndio sababu Mswada uliopita kabla ya huu umezungumzia maneno ya pensheni. Hii ni kwa sababu tunataka kuhepa ufukara. Kuhepa ufukara ni kupata utajiri. Isiwe ni Wabunge tu ndio wanautafuta utajiri huu. Ni lazima wananchi tunaowaongoza wafanye biashara, nao pia waweze kuishi maisha mazuri. Tumeona mabwana wakidharauliwa na mabibi zao kwa sababu hawana kitu. Leo wakifanya biashara kisawasawa, hata akiingia nyumbani anapata heshima kisawasawa kwa sababu analeta mahitaji na pia kuwasomesha watoto, na kadhalika. Kwa ajili ya muda, nitawapatia wenzangu nafasi ili waendelee kuchangia. Naunga mkono Mswada huu. Asante."
}