GET /api/v0.1/hansard/entries/1506881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506881/?format=api",
"text_counter": 385,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Mheshimiwa Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nampongeza Seneta Asige na Mheshimiwa Irene ambaye alikuwa na Mswada mwingine wa maana zaidi wiki hii hii. Mbali na kumuunga mkono, karibu nimuunge mikono na kichwa. Tuna tatizo ambalo ni la kihistoria. Kama mwenzangu alivyotanguliza, tulisoma wakati tofauti. Ilikuwa usome na ukariri uliyofundishwa. Haikuwa kuelewa. Ilikuwa kukariri. Iwapo uliweza kuzungumza ama kuandika uliyokariri, ulisemekana kuwa mtu mwerevu sana aliye na akili nyingi na afaaye kupita mitihani na hatimaye kupewa kazi. Tumeishi na hali hiyo kwa muda. Mpaka sasa, baadhi ya wazazi wanaishi katika fikra hizo. Kwamba ni lazima mtoto aende darasani kukariri. Kama ataweza kuzungumza au kuandika aliyokariri, basi huyo alidhaniwa kuwa mtoto mwema. Serikali imechukua hatua ya kuleta mtaala huu mpya uitwao Competency-Based"
}