GET /api/v0.1/hansard/entries/1506884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1506884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506884/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Hatuna upungufu wa ubunifu hapa Kenya. Kuna kijana amebuni vitu vingi sana katika Eneo Bunge langu la Matuga, pale Kombani. Ametengeneza stima, amebuni mfumo wa kusafisha wa hewa kama tulivyokuwa tunafanya wakati wa Corona ili tupate oksigeni na mambo kama hayo. Lakini mara nyingi watu au sisi ndio huwa na matatizo kwa sababu huona watu kama wale kama wasio na akili au wanafanya vitu visivyo vya kawaida kwa sababu hawajiwezi. Ni vitu hivyo visivyo vya kawaida huleta mafanikio na kuendeleza Kenya. Hatimaye, vitawezesha vijana kujisimamia. Kwa hivyo, Mswada huu ni wa maana sana kwa wakati huu. Tuna matatizo mengi. Tukiangalia tunakoelekea, sioni kama kuna wakati uchumi wa Kenya utaimarika. Hata ukiimarika, si watu wote wataajiriwa kwa kazi za kuanza saa mbili asubuhi na kuisha saa kumi na moja. Kwa hivyo, njia ni hii peke yake. Nina imani kuwa hakuna mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimleta hapa duniani akiwa hana maarifa aliyompatia. Tatizo ni kuwa tumejiweka katika njia moja tu, kwamba, ili uwe una maarifa, lazima uende shule, usome kemia, fizikia ama hisabati. Lakini Mwenyezi Mungu alimpatia kila mtu maarifa yake. Ombi langu ni kuwa ili Mswada huu uwe wa maana, taaasisi zingine za Serikali zianze kutadhmini kuwa kuna wale wanaoweza kuenda shule na wasifanye vizuri. Labda wana akili na maono mbadala, na wana ubunifu. Ndio maana naunga mkono Mswada huu ukilinganishwa na mtaala wa Competency-Based Curriculum (CBC) ulioko wakati huu."
}