GET /api/v0.1/hansard/entries/1506886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506886/?format=api",
"text_counter": 390,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Ikiwa Kenya hii itaendelea, ni lazima tuwapatie nguvu na kuwaheshimu wale wanaotaka kuanzisha vitu vipya. Ukitaka kunawiri katika biashara, ni lazima ulete vitu tofauti. Unaweza ukampata mtu aliyeanzisha biashara ambayo tayari ipo kama biashara ya duka, pikipiki ama texi. Hayo si malengo, na hayatatupeleka mbele. Kunapaswa kuwe na vijana walio na mawazo na uzoefu tofauti kuliko watu wengine. Hao ndio tunapaswa kulenga ili tuwapatie msaada na sehemu ambapo wanaweza kuanzisha biashara zao. Wanaweza kupata wataalamu watakaowaongezea fedha. Serikali inaweza kuingilia sio tu kwa kiwango cha kuwapatia fedha, lakini pia waangalie taaluma hiyo kwa sababu pengine haihitajiki hapa Kenya, lakini kuna nchi ughaibuni ambayo taaluma hiyo inaweza kusaidia. Je, wataweza kuwasaidia vijana hao kwa njia ipi ili mafikira na maono yao yawe ya maana zaidi?"
}