GET /api/v0.1/hansard/entries/1506887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1506887,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506887/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Kuna tatizo ambalo mara nyingi linawakumba wale walio na maono mazuri, tofauti na vile watu wamezoea. Serikali lazima iwe na jukumu la kuhakikisha kuwa wakati kijana ama mtu yeyote amekuja na mfumo mpya wa maana, atalindwa vipi kutokana na yale mashirika na kampuni kubwa kubwa ambazo zinaweza kulichukua jambo hilo na kujinufaisha. Nina mfano ambao nafikiria sisi sote tunaujua. Aliyeanzisha mfumo wa M-Pesa ulimwenguni hakuwa mtu aliyeajiriwa ama anayetoka kwa familia kubwa. Lakini papo hapo, mashirika ya pesa yalichukua fursa hiyo kununua maarifa ya yule kijana na kumlipa. Kijana huyo aliona kuwa amepata pesa nyingi bila kujua kuwa hatimaye, mfumo huo utatambulika ulimwenguni mzima na utaleta fedha nyingi ilhali yeye amebaki akilalamika kuwa hajanufaika zaidi."
}