GET /api/v0.1/hansard/entries/1506991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1506991,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1506991/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni Ya Kudumu No.53(1) ya Kanuni za Seneti kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Leba na Ustawi wa Jamii, kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya uzeeni ya wafanyikazi wa Shirika la Kenya Aerotech, waliostaafu. Bw. Spika, katika kauli hiyo- (1) Kamati itoe orodha ya majina ya wafanyikazi wa Shirika la Kenya Aerotech waliostaafu kutoka mwaka wa 2002 mpaka leo, ikionyesha ni wangapi wamepata malipo yao ya uzeeni na wangapi hawajapata. (2) Ieleze sababu za kucheleweshwa kwa malipo hayo kwa wafanyikazi waliostaafu, hususan Bw. Mohamed Abdala Harusi ambaye alistaafu mnamo 31/12/2022. (3) Ibaini ni lini wafanyikazi hao watapata malipo yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}