GET /api/v0.1/hansard/entries/1507039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1507039,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507039/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Spika, ningependa kuzungumza kuhusu taarifa aliyoleta Sen. Faki. Watu wanaofanya kazi kwa miaka mingi hawalipwi mapato waliokuwa wakiweka baada ya kustaafu. Mara nyingi tunaona watu waliokuwa katika mamlaka wakiishi maisha ya uchochole baada ya kustaafu. Wanaishi maisha mabaya kana kwamba hawakuwa na heshima wakati walipokuwa wakifanya kazi. Haya yote yanachangiwa na taasisi zinazoweka mapato ya wafanyikazi. Wanawafanyia madharau kwa sababu wanachukua pesa hizo na kufanyia kazi zingine. Sasa imekuwa kama mchezo. Kila mtu anayefanya kazi nchini Kenya hana uhakika kwamba pesa ambazo amekuwa akikikatwa ili kuwekwa kwenye hazina zitamfaidi wakati amestaafu na kumhakikisha maisha mema. Langu ni kwa wale wanaohusika na kuweka pesa za wafanyikazi, wakiwemo walimu na wafanyikazi wengine, imefika wakati wanafaa kuangaliwa. Kama kuna njia mbadala ya kuona kuwa wanalipwa mapato yao angalau mwezi mmoja au miwili kabla ya kustaafu, maisha yao yatakuwa sawa na kwenda sambamba jinsi walivyokuwa wakiishi. Bw. Spika, hayo ndiyo maoni yangu. Asante."
}