GET /api/v0.1/hansard/entries/1507067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1507067,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507067/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza naunga mkono taarifa kuhusu wakulima wa miraa. Ningependa kuwafahamisha kwamba kuna miraa inayotoka eneo la Meru na muguka kutoka kaunti za Embu na Kirinyaga. Wakati soko la hiyo bidhaa linatafutwa, ni vizuri wakulima hawa wawakilishwe. Tumeongea kuhusu wakulima wa miraa kwa sababu ni muhimu. Lakini ni vizuri pia tukae pamoja kama viongozi kuzungumzia usafirishaji wa miraa. Kama viongozi, tunafaa kuongea na wale wanaosafirisha miraa ama muguka kwa sababu wanasababisha harasa kubwa sana katika eneo la Kirinyaga. Wiki hii tumezika watoto wawili waliogongwa na gari linalosafirisha miraa. Kila mwaka takwimu inaonyesha wazi kwamba wale wanaobeba miraa na muguka katika eneo la Mwea wanaua watu zaidi ya 55. Sijui kazi ya polisi ni gani kwani kuna vilio kila mwaka kwa sababu ya watu wanaoendesha gari za kubeba miraa kwa kasi sana inayosababisha wengine kupoteza maisha yao. Kuna mmoja alikuwa yatima na tulikuwa tunatafuta mahali pa kumzika jana kwa sababu mahali pa makaburi pamejaa pia. Jambo hili litakuwa la maana na manufaa kwa mkulima wa miraa na muguka kama watatafutiwa soko na vilevile wenyeji wanaotumia barabara zetu wawe na haki yao ya maisha. Sio madereva wote ni wabaya, bali kuna baadhi ambao sijui shida yao ni nini. Wanaokula miraa hawana haraka ya kula miraa kwani utawapata wamekalia vigogo kwa masaa manne au matano wakitafuna miraa yao bila haraka wala wasiwasi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}