GET /api/v0.1/hansard/entries/1507074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1507074,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507074/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono taarifa iliyoletwa katika kikao hiki cha Seneti kuhusu miraa na muguka. Tumezungumzia mambo haya kwa muda mrefu na inaonekana bado kuna shida kwani bado tunayazungumzia hivi leo. Ningeomba siku zinazokuja, Kamati ya Agriculture, Livestock and Fisheries pamoja na Kamati ya Tourism, Trade and Industrialization na National Security, Defence and Foreign Relations zikae pamoja zione vile zitasaidia mkulima wa miraa na muguka. Wakulima kutoka Kirinyaga, Tharaka Nithi, Embu na Meru wanaendelea kulima miraa na muguka ilihali bei inaendelea kurudi chini kwa sababu ya vita ya hapa na pale. Ningeomba hata kama kuna kizuizi baina ya Somalia na nchi yetu, kamati hii iangalie kwa makini bei ya miraa nchini. Bw. Naibu Spika, mambo haya yanafaa yachunguzwe na kamati zote tatu ili mkulima afaidike. Tunajua kuwa watafuatilia bei ya miraa humu nchini na pia kwenye soko za nchi za ng’ ambo. Hili litafanya tujivunie kwa sababu tutakuwa na sheria inayofaa. Miraa inafaa kuwa kama cash crops zingine kam vile pamba, majani chai, kahawa na macadamia."
}