GET /api/v0.1/hansard/entries/1507094/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1507094,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507094/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii ambayo umenipa kuchangia. Mambo ya fedha za uzeeni ambazo wafanyikazi wanatozwa ni jambo nililotaja wiki iliyopita. Hili ni jambo la kusononesha sana. Bunge hili la Seneti limegeuzwa kuwa kinanda mbele ya Wakenya. Haiwezi kuwa leo ni santuri ya fedha za kustaafu, wiki ijayo kama, Bw. Naibu Spika, unaweka santuri ile ile. Sio vyema wala haki kwa Wakenya kutuona sisi kama walalamishi wasio na suluhisho. Naomba tutamatishe shughuli hii kwa kuuliza Serikali ya Kitaifa, watumishi wa umma pesa zao zipo ama hazipo? Viongozi katika kaunti - magavana watuambie, pesa za wafanyikazi zipo ama hazipo. Wanakatwa ama hawakatwi?"
}