GET /api/v0.1/hansard/entries/1507098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1507098,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507098/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ni kitendawili ama ni kinaya, hadi sasa kaunti yangu ya Bungoma pesa hazijafika. Wananiambia yule ambaye anastahili kuweka sahihi ili malipo yafanyike hayupo. Nami naomba anapopatikana, fedha ziende kwa wale ambao wanapaswa kulipwa. Kama ni wanakandarasi walipwe. Watu wasilipwe ilhali mradi unaenda kubadilishwa baada ya mwezi moja. Ni jambo la kustaajabisha kuwa serikali za kaunti zimeanza kucheza shere na Serikali ya Kitaifa hapa Nairobi. Unapata mwezi huu serikali ya kaunti inatoa shilingi 10 milioni kurekebisha muundo msingi fulani na baada ya miezi miwili, serikali ya Kitaifa inaweka pale shilingi 200 milioni. Sasa shilingi 10 milioni ni ya kusafisha halafu shilingi 200 milioni ni ya kufanya kazi? Huu ni utapeli na hatupaswi kuruhusu watu kutumia pesa kama hizi kujinufaisha wenyewe. Bw. Naibu Spika, najiunga na Maseneta wengine. Mambo ya mashamba na Wakenya ambao wanaenda nchi mbalimbali kutafuta kazi halafu wanaporwa pesa zao ni jambo ambalo hatutaruhusu."
}