GET /api/v0.1/hansard/entries/1507114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1507114,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1507114/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kukubali uteuzi wa Bw. Gerald Nyaoma kama Naibu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Kenya. Ripoti ya Kamati iko wazi kwamba Bw. Nyaoma alikuwa amehitimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alipata Shahada ya Bachelor of Arts kwa masuala ya arts. Vilevile akaenda Chuo Kikuu cha Cambridge ambapo alifanya vizuri na kupewa shahada maalum kwa sababu ya bidii yake ambayo ilimfanya kuwa mwanafunzi wa kwanza katika chuo kile mwaka huo. Vile vile amehitimu kama mhasimu yaani accountant. Amefanya kazi kwenye Benki Kuu zaidi ya miaka 30 mpaka alipostaafu hivi majuzi kama mkurugenzi wa masuala ya uangalizi wa Benki hiyo. Kama ilivyosemwa na Kamati ni kuwa Benki Kuu ya Kenya ni taasisi muhimu sana katika nchi yetu. Inasimamia uchumi wa nchi. Inasimamia fedha na hali nzima ya mchakato wa uchumi nchini. Kuwepo kwa uongozi ambao unatajiriba kubwa kama hii utasaidia pakubwa kuiendeleza benki hii ili uchumi wetu uweze kuimarika na kuwe na hali ambayo inawapa waekezaji confidence kwamba wakiwekeza hapa nchini ni vizuri na ni maendeleo kwa nchi yetu ya Kenya. Nchi yetu inataka wawekezaji hivi sasa, kwa sababu, masuala ya kuomba mikopo na misaada imepitwa na wakati. Ni lazima tulete wawekezaji ili uchumi wetu uweze kukua. Tuajiri watu wengi, kama vijana wanaomaliza vyuo vikuu na taasisi zingine ili uchumi uweze kuimarika. Ningegusia mambo mawili matatu ambayo nimeona yako katika uchumi wetu kwa sasa. Tumeona kuwa Benki Kuu imeshukisha Riba ya Mikopo ila benki nyingi, riba iko kwenye asilimia 23 na 20 wakati Benki Kuu imetoa mwongozo kuwa mikopo ishuke. Tunatarajia kwamba uteuzi wa Bw. Nyaoma kama Naibu Mkurugenzi wa Benki Kuu utasaidia pakubwa kusukuma hizi benki za biashara kupunguza riba ili wananchi wapate mikopo ya rahisi kisha watafanya biashara na kupanga maendeleo tofauti tofauti katika maeneo yao. Jambo la pili ni kuwa Bw. Nyaoma alikuwa msimamizi wa Benki wakati huduma ya Mpesa ilikuwa inasajiliwa kwa mara ya kwanza. Alijieleza kwa ufasaha kwamba alichukua jukumu la kupendekeza kwamba huduma ya Mpesa ipewe leseni. Baada ya hapo tumeona mabadiliko makubwa yamefanyika katika huduma za fedha za kidijitali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}