GET /api/v0.1/hansard/entries/1508016/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1508016,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1508016/?format=api",
    "text_counter": 771,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia Hoja hii muhimu sana, ambayo inaangalia biashara za kudhuru nchi nzima kiuchumi na pia vijana wetu. Ni lengo la Serikali ya Kenya Kwanza kupata wawekezaji haswa kwa upande wa uzalishaji, ili vijana wetu wapate kazi. Ni jambo la kuhuzunisha wakati tunazungumzia wawekezaji ambao hawaji hapa Kenya kuweka viwanda ili vijana waajiriwe, lakini wanakuja kufanya biashara kwa manufaa ya kutengeneza faida na kurejesha pesa kwao. Hoja hii ni muhimu na imekuja wakati unaofaa. Nchi inahitaji wawekezaji, lakini wawe ni wale ambao wanakuja kuwekeza kwa manufaa ya nchi na si kwa sababu ya biashara ya mtu binafsi ama ya shirika fulani la nchi za kigeni."
}