GET /api/v0.1/hansard/entries/1508018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1508018,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1508018/?format=api",
    "text_counter": 773,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Aliyetanguliza amezungumzia vizuri kuhusu Ripoti ya kamati ambapo waligundua kwamba hao wanafanya tu biashara na hela zote wanarejesha kwao. Hii ina maana kwamba, sisi hatupati faida yoyote ya maana. Ikizidi, wanarejesha kwao pesa za kigeni. Kwa hivyo, inazidi kupunguza ule mfuko wetu wa pesa za kigeni ilhali hatuna faida yoyote ya maana. Kama ilivyotangulizwa, katika uchunguzi wa wanabiashara wa China Square, hatuna matatizo katika ngazi za nchi kuhusu maelewano kati ya nchi za kigeni kama China. Hata hivyo, tufahamu kwamba hiyo ni nchi kubwa yenye rasilimali nyingi. Kwa hali yoyote, viwanda vyao vimeendelea sana kwa sababu ya wingi wa watu. Kwa wale ambao tumebahatika kuenda kule Uchina, utakuta kwamba kwa sababu hao tayari ni wengi, wana soko la kutosha na hatuwezi kamwe kushindana nao katika uzalishaji mali wakati soko letu ni ndogo. Pili, kwa sababu ya kuwa wao wameendelea pia kiteknolojia, wana mbinu mpya ya kuzalisha hizo bidhaa. Inamaanisha kwamba, endapo wewe utataka kuzalisha bidhaa ambazo zinafanana na mbao, kwa mfano, gharama yako ya kuzalisha moja kwa moja inatakuwa nyingi, bali kwao inakuwa ndogo, maana hao wana uwezo wa kutuletea kitu ambacho kinafanana na mbao. Kwa hivyo, wanakuwa na ile nafuu ya kutuuzia sisi ilhali sisi bidhaa yetu itakuwa ghali. Nasimama kuunga mkono Hoja hii na taratibu zilizozungumziwa ili tuweze kulinda rasilimali zetu na kupata wawekezaji watakaokuja kwa lengo la kutuletea faida na kutoa fursa za ajira kwa vijana. Ahsante kwa kunipatia fursa hii."
}