GET /api/v0.1/hansard/entries/1509278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1509278,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1509278/?format=api",
"text_counter": 908,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Cha msingi ni kwamba, ijapokuwa Seneti inafanya kazi yake, kuna mambo yanayofanyika yanayozidi kurejesha nyuma ugatuzi, kwa mfano, utendakazi wa serikali zetu za kaunti. Kuna malimbukizi ya madeni kila mwaka yanayosababisha hasara kwa kaunti zetu. Ikiwa kwa mwaka kaunti zinashindwa kulipa madeni na kuongeza mengine, ina maana kwamba yataendelea kuongezeka. Bi. Spika wa Muda, nachukua fursa hii pia kuwakaribisha nyote na Wabunge wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Kaunti ya Mombasa kwa michezo ya---"
}