GET /api/v0.1/hansard/entries/1509440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1509440,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1509440/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Sen. Kibwana; taarifa kuhusiana na siku 16 za kupambana na gender-basedviolence yani vita dhidi ya dhuluma ya kijinsia. Ni siku kumi na sita ambazo zinaadhimishwa kuanzia tarehe 25 mwezi uliopita mpaka tarehe 10 Decemba. Kwa kusema kweli, mwaka huu katika nchi ya Kenya, tumeona visa vimeongezeka vya ukatili dhidi ya wasichana, kina mama na vile vile pia watoto wadogo wa kike. Polisi walipotoa tarakimu zao mwezi uliopita, ilikuwa karibu wanawake 100 ambao walikuwa wameuliwa mikononi mwa watu kwa sababu za kikatili. Hilo ni swala ambalo kwa sasa Kenya ilifikia wakati ambapo kina dada wanapigania haki ya kutimiza thuluthi moja katika Bunge. Kupambana na kuwa wanapigwa kama hivyo, si jambo la kufurahisha. Kenya yetu ina Katiba ambayo inapaswa kufuatwa. Vile vile katika tamaduni zote za Wakenya katika makabila 47 au 48 kwa sasa, hakuna kabila ambalo lina tamaduni ya kuwaadhibu wanawake ama kuwapiga. Kwa hivyo masuala haya yameongezeka na nyingi hutokea kwa sababu ya zile vitu tunaita online. Watu wanaanza uhusiano usioeleweka katika mitandao na baaadaye unapata katika uhusiano huo kunatokea kifo ama kudhurika kwa yule mtoto wa kike. Kwa hivyo, tungependa kuisihi serikali kwamba swala hili liangaliwe. Sisemi kwamba hao watu 100 waliokufa ni wachache. Kwa sasa hata mtu mmoja akifa kwa njia ambayo si ya sawa, ni makosa katika Katiba yetu. Kwa hivyo, ni lazima tupambane na jangaa hili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}