GET /api/v0.1/hansard/entries/1509441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1509441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1509441/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika Taarifa ya pili ambayo nilikuwa nataka kuchangia ni taarifa ambayo imeombwa na Naibu wa Spika, Seneta wa gatuzi la Meru, kuhusiana na mambo yalivyo katika University of Nairobi ambacho ni chuo ambacho mimi niliwahi kupitia. Ni jambo la kusikitisha kwamba vyuo vyetu sasa vina kuwa ni mahali ambapo uongozi haufanyiki au uongozi umekuwa duni kiasi ambacho migogoro na mizozano haishi. Ikumbukwe jumatatu ya wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano ya wafanyikazi Kenyatta University Teaching and Refferal Hospital (KUTRH ) ambapo ikasabisha kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Jopo ya hospitali ile, Profesa Mugenda. Vile vile, mkurugenzi msimamizi Dr. Adan pia ikabidi aende nyumbani kutokana na hali ambayo ilikuwa hairidhishi katika chuo kile. Bw. Spika, KUTRH ni hospitali ambayo ni Level 6 na katika Kenya hospitali kama hizi ziko tatu pekee yake. Haipendezi kwamba taasisi kama ile ikumbwe na mgogoro wa uongozi wakati hapa Kenya tuna viongozi wakila aina. Tunaweza kuleta maprofesa wa kila aina. Kwa hivyo, inaonekana taasisi zetu zinaingia katika mikono ya uongozi ambao sio ya sawa. Hii ndio sababu ya hii migongano na migogoro ambayo haiishi katika taasisi zetu na vyuo vikuu. Moi University imekwenda na maji. Nilisikia Seneta wa Nandi akisema kwamba Moi University imesaidia Karatina University na vyuo vingine. Hata hivyo, vipi usaidie wengine wainuke halafu wewe mwenyewe uzame? Inatokana na uongozi mbaya. Kwa hivyo ni lazima kama Seneti tupambane na visa vya uongozi mbaya katika taasisi za kitaifa. Bw. Spika, tukizifungia macho kuwa ni watu wanaotoka kwetu, jamaa zetu ama University iko kwetu kwa hivyo lazima kiongozi, mwenyekiti ama Vice-Chancellor atoke kwetu ili aongoze taasisi kama ile, tutakuwa tunawaharibia Wakenya na vijana ambao wengi wana matumaini kwamba wakitoka katika University ile wataweza kutimiza ndoto zao za kufanyia kazi taifa la Kenya. Asante."
}