GET /api/v0.1/hansard/entries/1510359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1510359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1510359/?format=api",
"text_counter": 413,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kuba ni nchi ambayo kila mtu hapa duniani anajua kuwa wanasomesha watoto wao kutoka shule za chekechea hadi vyuo vikuu bila malipo yoyote. Ni kitu gani ambacho watu wa Kuba walifanya ambacho sisi hapa Kenya tunashindwa kufanya? Mjadala kuhusu Hoja hii unaashiria kwamba pesa zipo. Licha ya kuwa zaidi ya thuluthi moja ya bajeti ya Kenya inaenda kwa taasisi ya elimu, pesa hizo zimegawanywa kila mahali. Wizara ya Elimu inatoa basari. Kuna pesa nyingine inayotoka kwa mhe. Rais. Vile vile, magavana wana pesa---"
}