GET /api/v0.1/hansard/entries/1514206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1514206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514206/?format=api",
"text_counter": 589,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": "Nawapongeza Wajumbe wenzangu ambao wamechukua fursa ya kufanya mchakato mzima wa kukusanya zile sahihi ili tuweze kujumuisha masuala haya kwa Katiba. Pesa nyingi ambazo zimetengwa kwa ugatuzi hatuoni kazi zake. Kuna uzembe fulani katika kaunti nyingi. Wananchi wanalia kuhusu afya. Ni shida tupu. Hakuna madawa na hospitali zimezorota kabisa. Hata masuala ya maji yamekua shida mashinani. Fedha ambazo zimekua za manufaa sana ni NGAAF na NG-CDF. Niko katika mstari wa mbele ili tuweze kujumuisha mpango mzima huu ndio hata maseneta wapate fedha ya kuangalia vipi kaunti zetu zinaendeshwa. Naunga mkono."
}