GET /api/v0.1/hansard/entries/1514441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1514441,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514441/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwanza nachukua fursa hii kuwaambia Wabunge wote Happy New Year . La pili, Mhe. Spika, natoa rasmi rambirambi zangu kwa familia yako na ndugu yetu Mhe. Timothy, kwa kumpoteza mama yenu mzazi. Mwenyezi Mungu amhifadhi na wema. Nachukua fursa hii kuwapongeza wote ambao wameteuliwa kuhudumu kwenye tume ya SRC. Kama walivyoeleza wenzangu, namuomba Bw Sammy Chepkwony, akichukua kiti hiki, aangalie maslahi ya wakenya wote. Kama walivyosema wenzangu, Wabunge huwa tunapata mtihani mkubwa sana wakati tunapoongezwa mshahara. Ifahamike kuwa Mbunge ana kazi kubwa sana. Miongoni mwa Wabunge wote, nafikiri mimi ndiye maskini zaidi kwa sababu huwa natoa hela zote hadi nabaki bila ya hata sumuni. Wakenya wako na matatizo mengi. Mkenya anajua kwamba ataendea malipo ya hospitali kwa mama kaunti. Mwenye ako na msiba pia anaenda kwa mama kaunti. Mtu ambaye ako na tatizo lolote lile, anaenda kwa mama kaunti. Kuna mapya pia. Watoto wetu ambao wamepata nafasi za kwenda nchi za nje kutafuta kazi wanatufuata sisi Wabunge tuwasaidie. Na hawahitaji pesa kidogo. Mtu mmoja huwa anahitaji laki mbili au laki moja na nusu. Ndio maana ninasema wanaoshugulika na Youth Fund wachukue vijana hao wawape hizo pesa ili walipe wakishaenda, angalau tupunguziwe mzigo. Nawaambia makamishna hao kuwa wakenya wanahangaika sana wakati wa kupata mishahara yao, na jambo hilo limeleta hali ya sintofahamu. Yule Kamishna aliyetoka alitutangaza hadharani wakati ambapo Jumba hili lilikuwa limeingiliwa na Gen-Z na tukachomoka mbio. Bado tulikuwa tunayafikiria yale machungu tena tukawekwa kwenye gazeti kuwa tumeongezwa mshahara na Ksh7,000. Hiyo shilingi elfu saba ilifanya tukatukanwa mpaka mwenzangu akanilazamisha kwenye mkutano mmoja tukakatae hiyo nyongeza ya mshahara, ila tayari ilikuwa imeshawekwa kwenye sheria. Lakini maisha yetu yalikuwa hatarini. Wakenya wengi walikuwa hawafikirii kuwa huyu ni Mbunge na hana hili ama lile, anatusaidia hapa na pale kwa hivyo hiyo nyongeza ya Ksh7,000 sio kitu. Ilibidi twende mbio kwenye mikutano tuseme hatukubali hiyo nyongeza lakini ndani ya roho zetu, tulikuwa tunatamani hata tuongezewe zaidi kwa sababu mambo ni magumu. Ndani ya Bunge hili, tulipitisha Mswada wa wazee wa mitaa ambao wanafanya kazi kubwa sana kule mashinani. Hao ndio polisi na majaji. Wanajua ni mtoto wa nani amepotea. Pia wanajua ni nyumba gani watu wamepigana ili waende wasuluhishe. Wazee wa mitaa wanafanya kazi ngumu sana kushinda sekta nyingine zote. Tulipitisha hapa kuwa walipwe mshahara lakini hilo halijafanyika. Namuomba ndugu yetu Sammy Chepkwony na Tume yake wafikirie wazee wa mitaa ili nao wapewe angalau kitu kidogo kama wanavyofanyiwa Community Health Promoters (CHPs). The electronic version of the Official Hansard Report is for informationpurposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}