GET /api/v0.1/hansard/entries/1514442/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1514442,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514442/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Pia kuna madiwani wastaafu. Tulipitisha katika Bunge hili hapo awali kuwa wao pia wapate kiinua mgongo kidogo. Wananipigia simu kuzungumzia jambo hili. Hoja hiyo ilipita hapa Bungeni lakini haijakuwa effected na mpaka sasa hakuna kitu wanapata. Nawaomba makamishna hawa washikane na wakenya wote na wazingatie maslahi ya daktari, mwalimu, mbunge na mfanyi kazi yeyote wa Serikali kwa sababu gharama ya maisha imepanda sana. Kila wakati bei ya bidhaa ikiongezeka, mshahara uko pale pale. Kwa hivyo, wanapoongeza mshara, waangalie kutoka yule mfanyi kazi wa Serikali wa chini hadi yule wa juu. Wakipata kiinua mgongo kidogo, kitaweza kuwasaidia. Nawapongeza makamishna hawa na nawambia wafanye kazi ili wainue wakenya wote bila mapendeleo. Wasipendelee Wabunge kwa sababu sisi ndio huwa tunachapwa fimbo sana. Mishahara ya watu wengine ikiongezwa, huwezi kuona ikijadiliwa kwenye magazeti. Sijui huwa tumekosea kitu gani kwa sababu tunapigwa fimbo. Lakini unaporudi nyumbani, mtu ako na matanga utasikia: ‘Mama kaunti, tuko na msiba hapa.’ Wengine wanatuambia tuwasaidie mpaka birthday . Tukiongezewa mshahara, tunawaomba Wakenya watuelewe kwa sababu huwa tunaenda kwao na hizo pesa. Twala na wananchi. Hatuli peke yetu. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}