GET /api/v0.1/hansard/entries/1514575/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1514575,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514575/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ", nami pia naunga marekebisho haya. Kwa mfano, Wamaasai wamekuwa wakitengeneza bidhaa zao halisia hapa Kenya. Hata hivyo, bidhaa hizi hunuliwa na mataifa mengine na kupachikwa label zao na kuzirejesha nchini kwa bei ya juu sana. Tukipitisha marekebisho haya, basi ni watu wengi walio na uhalisia wa kutengeneza bidhaa watasaidika kwa kupata mapato yao kama ilivyokadiriwa. Si vyema watu wengine kufaidika kupitia ubunifu wa watu wengine. Wasanii nchini wanadhalilishwa. Kwa mfano, katika mataifa mengine, nyimbo huwekwa copyright lakini huku kwetu wasanii wanaobuni nyimbo hizo hawafaidiki kwa sababu watu wengine wanachukua nyimbo hizo na kuzimiliki. Kwa hivyo, naunga mkono ili tuweze kuwalinda wasanii wetu kupitia Mswada huu."
}