GET /api/v0.1/hansard/entries/1515155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1515155,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515155/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Zamzam Mohammed (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mombasa County, ODM): Asante Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuunga mkono hawa walioteuliwa. Kwanza ninampongeza dada yetu, Mwanamaka Amani Mabruki, anayetoka katika jimbo la Mombasa. Ni mwanamke ambaye ni msomi, mpole, mchapakazi, na ambaye ameweza kuhudumia Public Service miaka mingi. Huyu ni mtu ambaye tunamuamini. Ninataka kuwaambia wote walioteuliwa, Mhe. Spika, kuwa waweze kuhudumia jamii bila kuwa na mapendeleo. Nikimwangalia huyu Harun Maalim, amekuwa ni mtetezi sana wa watu wanaoishi na ulemavu, na nina imani nafasi hii ambayo amepewa itamwezesha kuhudumia walemavu kwa njia iliyo sawa. Sijui mambo ya Mwenyekiti na naibu wake, lakini kama ni kweli, Mhe. Spika, ijapokuwa majina hayako hapa, ingekua vizuri kama naibu wake angekua anatoka sehemu nyingine ili tuweze kuchanganya. Lakini hata hivo yule ambaye anaweza kupewa kazi, apewe na afanyie Wakenya wote kazi. Asante Mhe. Spika."
}