GET /api/v0.1/hansard/entries/1515237/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1515237,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515237/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Basi, asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii mimi pia niunge mkono uteuzi wa Mawaziri hawa watatu ambao walipitishwa na Kamati ya Uteuzi hivi majuzi na kuletwa katika Bunge hili leo hii. Ninaunga mkono tu na kuwapa Mawaziri hawa nasaha yangu kidogo. Ndugu zangu, mmechaguliwa. Pia, tunawachagua sisi kama Wabunge wa Bunge la Taifa kwa roho moja. Mimi ninatoka Kwale. Mnapofanya kazi, Mawaziri wetu, ningependa na ninaomba mjue Kwale pia ni kaunti kati ya zile kaunti arubaini na saba. Mnyoshe mkono kwetu pia. Mhe. Spika, Kwale ni kaunti iliyo na ukulima na mashamba yaliyo na rotuba nyingi sana. Sisi Wakwale pia ni wafugaji wazuri sana. Hata hivyo, utapata mara nyingi hatuwezeshwi katika ukulima na ufugaji wetu katika Kaunti yetu. Hatuwezeshwi kisheria na kifedha. Bado tunafanya ukulima ule wa zamani ambao hauwezi kwa sasa. Ulimwengu umefika mahali tunahitaji ukulima wa kisasa. Bado sisi tuko nyuma sana kwa mambo ya ukulima na ufugaji. Tunafuga kama nilivyoeleza. Nilikuwa na matumaini makubwa sana wakati Mhe. Salim Mvurya alichaguliwa katika Wizara hii ya Investment and Trade. Nilikuwa na matumaini nikijua kila mtu anajua mahali kiatu kinamchoma. Mhe. Mvurya angekuwa mzuri sana kwa kurekebisha Kwale. Kwa sababu hawa pia ni Wakenya wenzetu, ninawapatia kongole. Lakini waangalie sana Kwale kwa kuwa sisi hatuna viwanda. Base Titanium imeenda, inakufa. Mambo yake yamekwisha. Tuko na Ramisi Sugar Factory, ile iitwayo Kwale International Sugar Company Limited. Hatuwezi kusema tuna kampuni ya sukari Kwale. Hatuna viwanda ndani ya Kwale kabisa. Mawaziri, mnapoingia, nasaha yangu ni kuomba mjue Kwale pia ni kati ya zile kaunti arubaini na saba. Mtunyoshee mkono. Asante sana Mhe. Spika. Sitaki niseme kwa urefu sana. Ninaunga mkono uteuzi wa Mawaziri hawa."
}