GET /api/v0.1/hansard/entries/1515260/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1515260,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515260/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Asiache Mkenya yeyote nje. Sisi ni Wakenya pia. Kule kwetu Lamu ni mbali na kidogo tunasahaulika. Kwa hivyo, atuzingatie na atumie ile affirmative action kufikiria na kusaidia watu walio sehemu mbali mbali. Si lazima Lamu pekee, lakini Wakenya wote kwa jumla. Ningependa pia kumwambia Waziri wa Kilimo na Mifugo kwamba masuala ya samaki yako kwenye kilimo pia. Asiangalie tu upande wa kulima mimea pekee, bali pia aangalie mifugo na samaki. Aje na mbinu za kisasa zile ambazo zitatusaidia. Tusibaki kwenye hali ya babu zetu ambao walienda kuvua samaki na kupata pengine kilo ishirini tu. Saa hii, watu wanapoenda kuvua wanapata kilo moja tu. Atafute mbinu mbadala na za kisasa ili kusaidia wavuvi wetu waweze kufaidika."
}