GET /api/v0.1/hansard/entries/1515289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1515289,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515289/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika. Ninachukua fursa hii kukupongeza na kuombea kila mtu mwaka mpya mwema wa 2025. Twaomba ushirikiano kwa kufanya kazi pamoja. Ninawapongeza wateule hawa watatu. Nikizungumzia Mhe. Kabogo, sijafanya kazi karibu naye. Lakini kwa sababu ameteuliwa katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, ombi langu kwake ni ashirikiane na Wakenya wote, haswa vijana. Anaingia wakati vijana wako vyema kidijitali. Hatutataka waendelee kutumia mitandao vibaya. Aone vipi atatafutia vijana wote wanaohangaika na kusumbuka kazi za kidijitali. Wanasema wanachosema kwa sababu hawana kazi. Kuna kazi nyingi za kidijitali anazoweza kuwatafutia ili waweze kujikimu. Nilimjua Mhe. Mutahi Kagwe akiwa Waziri wa Afya. Saa hizi amepelekwa katika Wizara ya Maendeleo ya Kilimo na Mifugo. Pale alipo anisikie. Ninaitwa Mhe. Mbeyu wa Kilifi. Tunataka turejeshewe mimea ya pwani kama mkorosho na minazi. Japo kazi ya kilimo imegatuliwa, aweze kushirikiana na Serikali ya Kaunti ya Kilifi tuone vipi biashara ya mkorosho, maembe na nazi zinaweza kupata faida."
}