GET /api/v0.1/hansard/entries/1515752/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1515752,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515752/?format=api",
"text_counter": 370,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante Mhe. Spika. Tunaheshimu uamuzi wa korti lakini hatukubaliani nao. Mwanzo, sisi kama Jubilee Party, tulikuwa tushaenda. Hatuko kwa Azimio la Umoja-One Kenya Coalition Party. Ukiangalia Mawaziri wale tuko nao saa hii, ambao walipeleka haya mambo kortini, Mhe. Wandayi na Mhe. Mbadi, saa hii wako kwenye hii Serikali. Kwani hao mahakimu hawaoni mambo yamepita na yameendelea? Kwani wanaishi Kenya gani? Sasa huku ni kuleta taharuki. Sisi hatuna haja nayo. Serikali hii imepitia changamoto kubwa na nyingi. Kwa hivyo, tafadhali, tunaomba watupatie nafasi tuendelee. Kuna jambo kuhusu ofisi ya Mhe. Spika. Katiba haijasema Jambo kulihusu na imenyamaza. Hii yamaanisha inaruhusiwa. Haina haja kuwalenga Maspika wawili hawa. Katiba iko na ifuatwe. Haikukataza. Inamaanisha ni sawa uwe hapo kama Spika. Mhe. Spika, naona mlengwa ni wewe na labda utuambie ukweli. Hatujui umefanya nini huko. Ulikanyaga waya au kuna stori gani huko? Naona kama wewe ni mlengwa na sisi twaona haya mambo ni kama kumwambia bibi na bwana waliooana kwamba hawaruhusiwi kisheria kuonana ilhali wamependana na washazaa. Tumeshikana katika broad-based government . Sasa, shida zote hizi ni za nini?"
}