GET /api/v0.1/hansard/entries/1515766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1515766,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1515766/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Which one? Asante sana Mhe. Spika. Kwa sababu mimi ni mhandisi, sikumbuki ni mwandishi yupi aliyesema haina haja uendelee kubembeleza farasi wako unayempenda na anayekimbia mbio kushinda wengine na kuleta zawadi zote. Kwa bahati mbaya, umri wake hufika akafariki. Haina haja uendelee kumbembeleza na kumletea chakula kwa sababu ulimpenda sana ukidhani ataamka kukushindia mbio ulizotaka. Cha kufanya ni kutafuta farasi mwingine, umlishe, umfanyishe mazoezi, na aendelee kushinda. Sasa, kwa kifupi, uamuzi huu umepitwa na wakati. Najua wanahistoria ni wengi hapa. Ndio maana tunazungumza kwa kirefu. Sidhani kama kuna mtu aliye na tashwishi na ukweli ulivyo kwamba Azimio ilifariki. Kama hawataki kuizika, ni sawa. Lakini tunajua ilifariki. Uamuzi unazungumzia Azimio ambayo haipo. Sasa tutafufua vipi farasi ambaye amefariki hata kama tulikuwa tunampenda? Ndugu zangu, tukubaliane tulichagua Spika sawasawa. Kiongozi wa Walio Wengi ni Kimani Ichung’wah ambaye yuko hapa. Tukubaliane kuwa bado sisi ndio wengi. Sioni haja kudhani tutafufua farasi. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}